Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Ulisikia wito wa kumgeukia Mungu? Mifano mitatu ya m.14 husaidiana kueleza maana yake: Kuamka kutoka usingizi, kufufuka kutoka wafu, na kutoka gizani na kuingia nuruni kwa Kristo. Kwa nini Wakristo waenende kama ilivyostahili wito wao huo? Kwa sababu zamani walikuwa “giza,” sasa wamekuwa nuru katika Bwana. Kwa hiyo tuenende kama “watoto wa nuru” (m.8,Sasa mmekuwa nuru katika Bwana; enendeni kama watoto wa nuru)! Maisha ya zamani ya giza hayakuzaa matunda mazuri, ni kama kuishi bure (m.11, ...matendo yasiyozaa ya giza). Lakini Kristo akituangaza, matunda mazuri yapo! Rudia na kutafakari m.9,Tunda la nuru ni katika wema wote na haki na kweli.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/