Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Twatakiwa kumfuata Mungu kama watoto wake wapendwa. Tumtazame Kristo (m.2,Mkaenende katika upendo, kama Kristo naye alivyowapenda ninyi tena akajitoa kwa ajili yetu, sadaka na dhabihu kwa Mungu, kuwa harufu ya manukato)! Mapenzi ya Mungu ni mume mmoja na mke mmoja kuishi pamoja katika ndoa. Tujihadhari na hali zinazopinga! ”Kutamani” (m.3) kumewekwa pamoja na uasherati na uchafu, ikimaanisha kuvuka mpaka wa uhalali katika matumizi ya mwili. Wanaoishi upande wa pili wa mpaka huo aliouweka Mungu, hawatarithi ufalme wake (m.5,Hakuna mwasherati wala mchafu wala mwenye tamaa, ndiye mwabudu sanamu, aliye na urithi katika ufalme wa Kristo na Mungu). Waumini wasishirikiane nao (hii haina maana kujitenga naomaana hapo ingewalazimu kutoka katika dunia, kama ilivyoandikwa katika 1 Kor 5:9-10). Tujichunguze hali ya usafi wetu kiroho.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/