Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 17 YA 28

Haitoshi kutokusema uongo, hata tusinene neno lolote baya. Yawezekanaje? Tumvae Kristo! Tunene neno jema la Yesu analotukumbusha Roho Mtakatifu. Tunene mambo mazuri yenye faida na msaada kwa wale wanaohitaji mashauri na uongozi. Na zaidi maneno yetu yawe ya kuwahudumia wengine, yawe ya neema (m.29,Neno lo lote lililo ovu lisitoke vinywani mwenu, bali lililo jema la kumfaa mwenye kuhitaji, ili liwape neema wanaosikia).Wala msimhuzunishe yule Roho Mtakatifu wa Mungu; ambaye kwa yeye mlitiwa muhuri hata siku ya ukombozi(m.30). Dhambi zilizotajwa katika m.31 (uchungu, ghadhabu, hasira, kelele na matukano)zinamhuzunisha Roho Mtakatifu, maana zinaharibu ule umoja wa jamii ya kikristo aliouleta. Tumfurahishe Roho Mtakatifu kwa kuepuka dhambi hizo.

siku 16siku 18

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/