Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Mkristo amepewa utu mpya, basi avue wa zamani. Kuna tabia zipi za kuachwa? 1)Uongo. Tumewekwa huru na ukweli. Ni viungo katika mwili mmoja wa Kristo, kwa hiyo tuseme kweli sisi kwa sisi ili mwili ufanye kazi vizuri. 2)Hasira. Ni haki tukasirike, lakini vilevile ni haki yetu kumtwika Kristo hasira yetu. Basi, jua lisichwe na uchungu wetu. 3) Wizi. Ni badiliko kubwa kwa mwibaji kuwa mfadhili, lakini katika Kristo inawezekana afanye kazi, hata awe na ziada ili awasaidie wahitaji. Tumvae Kristo!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/