Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 15 YA 28

Waumini wamepewa maisha mapya badala ya yale ya zamani, basi waishi hivyo! Ni onyo zito, kwa sababu iwapo wameuitika wito wa kumfuata Kristo, bado wangali wamezungukwa na watu wanaonia kufuata desturi za maisha ya zamani bila kumjali Mungu. Watu hawa hawana ufahamu wa kweli kwa sababu tamaa zao huwadanganya na kuwatia giza. Wanaishi bila shabaha, na bila tumaini. Namna gani Wakristo waachane na maisha hayo? Wafanywe upya nia zao. Huanza na kupokea aliyowaumbia Mungu. Hebu tafakari upya huu ukirudia m.23-24,Mfanywe wapya katika roho ya nia zenu; mkavae utu mpya, ulioumbwa kwa namna ya Mungu katika haki na utakatifu wa kweli.

siku 14siku 16

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/