Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Lengo la Mungu ni kuwa na Kanisa lenye umoja wa imani na ufahamu wa Kristo (m.13,hata na sisi sote tutakapoufikia umoja wa imani na kumfahamu sana Mwana wa Mungu). Maisha ya waumini yafungamane na Kristo, kiasi cha hao kufikia utimilifu wake mwenyewe. Huku ni kukomaa na kujazwa na baraka na vipawa na neema ya Kristo. Wakristo wanatakiwa kusonga mbele ili waendelee kukua kiroho katika ufahamu wao wa Kristo. Wasiwe “watoto wachanga” wasioweza kusimama imara wakiyumbishwa na mafundisho ya uongo (m.14,Tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu). Je, unafikiri ni kwa kiasi gani umesimama imara katika Kristo?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/