Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Wakristo huwa na tofauti katika vipawa na huduma zao katika mwili wa Kristo (m.7,Kila mmoja wetu alipewa neema kwa kadiri ya kipimo cha kipawa chake Kristo). Mungu katika hekima yake amekusudia ziwepo tofauti hizo. Vipawa vyatoka kwa Kristo aliyepaa kama mshindi kabisa. Ndiye yuleyule aliyeshuka hapo duniani (m.8-9, Kristo ... alipopaa juu aliteka mateka, akawapa wanadamu vipawa. Basi neno hilo, Alipaa, maana yake nini kama siyo kusema kwamba yeye naye alishuka mpaka pande zilizo chini za nchi?). Vipawa hivyo hufungamana na huduma mbalimbali, k.mf. Mitume, Manabii, Wainjilisti, Wachungaji na Waalimu (m.11,Naye alitoa wengine kuwa mitume, na wengine kuwa manabii; na wengine kuwa wainjilisti na wengine kuwa wachungaji na waalimu). Kazi zote zina lengo moja la kuwakamilisha watakatifu na kujenga mwili wa Kristo. Twatakiwa kutumia vipawa tulivyopewa kwa kujenga Kanisa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/