Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Paulo anajiitamfungwa katika Bwana(m.1,Mimi niliye mfungwa katika Bwana), kwa sababu maisha yake yanatawaliwa na Yesu. Mungu ametuchagua kuwa watoto wake (1:4-5,Alituchagua katika [Kristo] kabla ya kuwekwa misingi ya uliwengu, ili tuwe ... watu wasio na hatia mbele zake katika pendo. Kwa kuwa alitangulia kutuchagua, ili tufanywe wanawe kwa njia ya Yesu Kristo, sawasawa na uradhi wa mapenzi yake), basi tumfuatekama watoto wanaopendwa(5:1). Tabia nne zitakazosaidia kuudumisha umoja wetu ni unyenyekevu, upole, uvumilivu na kuchukuliana katika upendo. Lengo la kuishi kwa tabia hizo sikuundaumoja balikuuhifadhi umoja wa Roho. Huo umoja umefafanuliwa kwa kutumia neno “moja” mara saba katika m.3-6 (Mwili mmoja, na Roho mmoja, kama na mlivyoitwa katika tumaini moja la wito wenu. Bwana mmoja, imani moja, ubatizo mmoja. Mungu mmoja). Katika maisha yetu tunatakiwa kuishi kwa tabia hizo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/