Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

SIKU 11 YA 28

Katika maombi twamkaribia Mungu kama Baba. Neno hili litutie moyo wa kusogea karibu naye (m.14,Kwa hiyo nampigia Baba magoti). Paulo anawaombea Wakristo wafanywe imara katika imani yao. Tumaini lao liwe kuwa Mungu ni tajiri wa utukufu. Nguvu yao itokane na kazi ya Roho ndani yao (m.16,awajalieni ... kufanywa imara kwa nguvu, kwa kazi ya Roho wake katika utu wa ndani). Na kwanza kabisa na hata mwisho, Kristo akae mioyoni mwao kwa wingi wote wa upendo wake. Upendo ndio kiini cha kumfahamu Mungu. Upendo wake katika Kristo ni mwingi sana kiasi cha kupita uwezo wetu wa kuufahamu. Mungu hujibu maombi.

siku 10siku 12

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022

Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/