Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Paulo aliona mahubiri yake yanawaangaza watu. Nje ya Kristo watu wamo gizani, hawana nuru ya ufahamu juu ya Mungu na makusudi yake. Wana haja ya kuufahamuutajiri wake Kristo(m.8b,nalipewa neema hii ya kuwahubiri Mataifa utajiri wake Kristo usiopimika). Kwanza wajue wokovu ni wa neema. Pili wajue kwamba wokovu huo ni sawa kwa Wayahudi na mataifa mengine yote. Tatu watambue kwamba Mungu aliyeviumba vitu vyote, sasa anaumba uumbaji mpya, na kwa uumbaji huo vitu vyote vitaletwa pamoja katika Kristo. Kanisa ni la muhimu katika utekelezaji wa mpango wa Mungu (m.10,Kwa njia ya kanisa, hekima ya Mungu iliyo ya namna nyingi ijulikane na falme na mamlaka katika ulimwengu wa roho).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/