Soma Biblia Kila Siku Februari/ 2022Mfano
Kabla ya tendo la Mungu, kila anayezaliwa amekufa kiroho na kutengwa kutoka kwa Mungu ambaye ni uzima na chanzo cha uzima (m.1,Nanyi mlikuwa wafu kwa sababu ya makosa na dhambi zenu). Wasioamini wamejielekeza kwa maisha yadunia hii mbovu iliyopo sasa(Gal 1:4). Hivyo niwatoto wa hasira, yaani hasira ya Mungu ambayo katika ukamilifu wake anaonyesha dhidi ya waliomkosea. Lakini wakati huo huo Mungu katika ukamilifu wake anatupenda. Siyo kwa sababu ya matendo yetu mema bali kwa sababu ndiye upendo. Je, uko tayari kuupokea upendo huu mkuu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Februari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Februari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Waefeso. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kushukuru Soma Bible kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/