Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Muda ule Yakobo aliotakiwa kumtumikia Labani ulikuwa unaelekea kwisha. Akawa na hamu ya kuondoka na kuanza kujitegemea mwenyewe. Ila Labani hakupenda aondoke: Iwapo nimeona fadhili machoni pako, kaa, maana nimetambua ya kwamba Bwana amenibariki kwa ajili yako (m.27). Ni bahati sana kukaa karibu na mtu aliyebarikiwa na Bwana! Katika Biblia tunapata mifano ya watu waliobarikiwa kwa njia hiyo. Mfano wa kwanza ni habari ya mwanamke huko Sarepta aliyempokea na kumhudumia Eliya kwa chakula. Mungu alimsaidia katika kipindi kigumu cha njaa (unaweza kusoma 1 Fal 17:9-16). Mfano wa pili ni habari ya mlinzi wa gereza walipokuwa wamefungwa Paulo na Sila. Kwa njia ya nyimbo, sala na Neno la Mungu akampokea Yesu, yeye pamoja na nyumba yake (soma Mdo 16:23-34 ukipenda)! Hata sasa Mungu hajaacha kutubariki tukiwa karibu naye. Tukiamini tutabarikiwa.
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/