Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano
![Soma Biblia Kila Siku Januari/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F29514%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Raheli alikuwa ameviiba vinyago vya babaye (m.19). Ila Yakobo hakujua ya kwamba Raheli ameiiba (m.32). Hii inaonyesha udhaifu wa imani ya Raheli. Hakumtegemea Mungu peke yake bali pia miungu. Tendo hili lilimpa Labani nguvu. Alifikiri amepata sababu ya kumshitaki Yakobo (m.30, Mbona basi umeiiba miungu yangu?). Lakini akafanyiwa ujanja na binti yake, Raheli (m.34-35, Raheli alikuwa amevitwaa vile vinyago ameviweka katika matandiko ya ngamia, na kuvikalia. Labani akapapasa hema yote wala hakuviona). Bila shaka alikuwa amejifunza ujanja kwa baba yake! Basi Labani akashindwa kuviona. Ndipo Yakobo akakasirika na kumwambia ukweli mjomba bila kuogopa (m.41-42, Miaka hii ishirini nimekaa nyumbani mwako; nilikutumikia miaka kumi na minne kwa binti zako wawili, na miaka sita kwa wanyama wako, nawe umebadili mshahara wangu mara kumi. Kama Mungu wa baba yangu, Mungu wa Ibrahimu na Hofu ya Isaka, hangalikuwa pamoja nami, hakika sasa ungalinifukuza mikono mitupu. Mateso yangu na kazi za mikono yangu Mungu ameziona, akakukemea usiku huu)!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku Januari/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F29514%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/