Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano
Bado Labani hakutaka kukubali kwamba ni haki Yakobo kuondoka na binti zake na mali nyingine (m.43, Labani akajibu, akamwambia Yakobo, Hao binti ni binti zangu, na wana ni wanangu, na wanyama ni wanyama wangu, na yote uyaonayo ni yangu). Lakini Mungu alikuwa amemwonya katika ndoto kwamba asimfanyie Yakobo ubaya wo wote (m.24, Mungu akamjia Labani, Mshami, katika ndoto ya usiku, akamwambia, Ujihadhari, usimwambie Yakobo neno la heri wala la shari; ling m.29). Hivyo alilazimishwa kupatana na Yakobo, na wakafanya agano (m.44-46). Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake. "Hofu ya Isaka" ni jina la Mungu. Kwa jina hili Yakobo alikiri kwamba Mungu ni Mtakatifu na ndiye ahukumuye. Je, una hofuya Mungu? Jichunguze na ujipime unaposoma mistari hii, Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, lakini vitu vyote vi utupu na kufunuliwa machoni pake yeye aliye na mambo yetu (Ebr.4:13). Na kama vile watu wanavyowekewa kufa mara moja, na baada ya kufa hukumu (9:27). Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai (10:31).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/