Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Katika kushughulikia tatizo la Dina Yakobo alionekana kama mdhaifu: 1. Aliwaogopa wenyeji (m.30, Yakobo akawaambia Simeoni na Lawi, Mmenitaabisha, kunifanya ninuke vibaya kati ya watu wa nchi hii, Wakanaani na Waperizi; na mimi, kwa kuwa watu wangu ni haba, watanikusanyikia, na kunipiga, nami nitaangamizwa, mimi na nyumba yangu). Kwa hiyo aliwasubiri kwanza wana wake warudi kutoka nyikani (m.5, Wanawe walikuwako pamoja na wanyama wake nyikani. Yakobo akanyamaza, hata walipokuja). 2. Hao walipokuwa wamefika, Yakobo akawaachia wao kuongoza mazungumzo (ukipenda, rudia m.13-17)! Wala hakuwapinga katika uamuzi wao. Huenda hakutambua hila yao. Ila baada ya mauaji kufanyika akawalaumu Simeoni na Lawi. Tendo walilolitenda ni baya, walitenda dhambi ya mauaji; waliua watu na wanyama! Ila kama Yakobo angeliwasimamia wana wake huenda yasingelitendeka!
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/