Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 23 YA 31

Yakobo akaondoka, akapandisha wanawe na wakeze juu ya ngamia ... ili afike kwa Isaka babaye katika nchi ya Kanaani ... akamhadaa Labani, Mshami, kwa kuwa hakumwambia ya kwamba anakimbia (m.17-18 na 20). "Kumhadaa" maana yake ni kumdanganya au kumfanyia ujanja. Ilikuwa hatua ngumu sana kwa Yakobo. Tusisahau kwamba Labani ni mjomba wake! Lakini alipata nguvu na ujasiri, maana Mungu mwenyewe alimwagiza kuondoka (m.3 na 13, Bwana akamwambia Yakobo, Urudi mpaka nchi ya baba zako na kwa jamaa zako, nami nitakuwa pamoja nawe … Sasa ondoka, toka katika nchi hii, urudi mpaka nchi ile uliyozaliwa). Tena Lea na Raheli wakamwunga mkono (m.14-16, Raheli na Lea wakajibu, wakamwambia, Je! Imetubakia sehemu au urithi katika nyumba ya baba yetu? Hakutufanya kama wageni, maana ametuuza, naye amekula fedha zetu kabisa? … Basi yo yote Mungu aliyokuambia, uyafanye)!

siku 22siku 24

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/