Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 26 YA 31

Bwana, uliyeniambia, Rudi uende mpaka nchi yako ... mimi sistahili hata kidogo hizo rehema zote ... Uniokoe sasa na mkono wa ndugu yangu, mkono wa Esau, maana mimi namwogopa ... nawe ulisema, Hakika nitakutendea mema (m.9-12). Kwa mara ya kwanza twamkuta Yakobo akisali. Ni kwa sababu alimwogopa sana Esau (m.6-7, Esau anakuja kukulaki, na watu mia nne pamoja naye. Ndipo Yakobo akaogopa sana, na kufadhaika sana) ambaye alilazimika akutane naye sasa. - Hapa twajifunza jambo muhimu kuhusu namna ya kuomba. Tuombapo tumkumbushe Mungu juu ya ahadi zake katika Biblia (ling. Yakobo anavyosema "uliyeniambia" katika m.9)!

siku 25siku 27

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/