Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano
Yakobo alisema, Baba yenu amenidanganya, akabadili mshahara wangu mara kumi; lakini Mungu hakumwacha kunidhuru ... Hivi Mungu akamnyang’anya mali yake baba yenu, na kunipa mimi (m.7 na 9). Labani alikuwa amepata mali nyingi na kubarikiwa kwa sababu ya Yakobo. Lakini hakugeuza moyo wake umwelekee Mungu. Hakumpa Mungu utukufu. Badala ya kuijali bahati yake akaiharibu kutokana na tamaa yake ya kupata hata mali zaidi. Jinsi alivyozidi kudanganya ndivyo umaskini ulivyozidi! Tujihadhari kupenda mali kuliko kumpenda Mungu. Kwa maana hatukuja na kitu duniani, tena hatuwezi kutoka na kitu... maana shina moja la mabaya ya kila namna ni kupenda fedha; ambayo wengine hali wakiitamani hiyo wamefarakana na Imani, na kujichoma kwa maumivu mengi (1 Tim 6:6-10).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/