Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 20 YA 31

Raheli alimwonea ndugu yake wivu. Akamwambia Yakobo, Nipe wana; kama sivyo, nitakufa mimi. Yakobo akamghadhibikia Raheli, akasema, Je, mimi ni badala ya Mungu? (m.1-2). Raheli hakuwa mcha Mungu kama Lea. Badala ya kumwambia Mungu tatizo lake akamwambia Yakobo akimlaumu. Ila baadaye alijifunza kumtegemea Mungu zaidi (m.22-24, Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu. Akamwita jina lake Yusufu, akisema, Bwana aniongeze mwana mwingine)! Kuwa na mke zaidi ya mmoja kulifanya nyumba ya Yakobo kukosa raha! Yesu Kristo anataka ndoa ya mume mmoja na mke mmoja. Anasema, aliyewaumba mwanzo, aliwaumba mtu mume na mtu mke, akasema, Kwa sababu hiyo, mtu atamwacha babaye na mamaye, ataambatana na mkewe; na hao wawili watakuwa mwili mmoja? Hata wamekuwa si wawili tena, bali mwili mmoja. Basi aliowaunganisha Mungu, mwanadamu asiwatenganishe (Mt 19:4-6).

siku 19siku 21

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/