Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano
![Soma Biblia Kila Siku Januari/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F29514%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Yakobo akampenda Raheli kuliko Lea (m.30). Lea akapata mimba akazaa mwana, akampa jina lake, Reubeni, maana alisema, Kwa kuwa Bwana ameona teso langu; sasa mume wangu atanipenda (m.32). Lea alikuwa amepata tatizo. Alikuwa anateseka kwa vile Yakobo alimpenda Raheli zaidi. Lakini akamkabidhi Bwana tatizo lake. Na Bwana akamsaidia na kumfariji! Kwa hiyo kila alipompata mwana alimpa Bwana utukufu! - Je, msomaji, unafikiri Mungu haoni tatizo lako au teso lako? Sikiliza anavyotualika akisema, ... nyenyekeeni chini ya mkono wa Mungu ulio hodari, ili awakweze kwa wakati wake; huku mkimtwika yeye fadhaa zenu zote, kwa maana yeye hujishughulisha sana kwa mambo yenu (1 Pet 5:6-7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
![Soma Biblia Kila Siku Januari/2022](/_next/image?url=https%3A%2F%2Fimageproxy.youversionapi.com%2Fhttps%3A%2F%2Fs3.amazonaws.com%2Fyvplans%2F29514%2F1280x720.jpg&w=3840&q=75)
Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/