Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano
Yakobo na ndugu zake walifurahi sana kuonana! Bila shaka ilikuwa mara ya kwanza wao kuonana, maana Harani ni mbali sana na nchi ya Kanaani (km 750 hivi). Ni kama kutoka Dar es Salaam mpaka Mbeya au kutoka Iringa mpaka Arusha! Na tukumbuke kwamba wakati ule hawakuwa na ndege au magari ya moto na wala treni au baisikeli. Sana sana walitumia kusafiri kwa punda, farasi au ngamia. Lakini wengi walitumia miguu tu. Na ndivyo Yakobo alivyosafiri! Maana alikuwa mkimbizi (27:43, Uondoke, ukimbilie kwa Labani, ndugu yangu huko Harani. 28:10-11, Yakobo akatoka Beer-sheba, kwenda Harani. Akafika mahali fulani akakaa huko usiku kucha, maana jua lilikuwa limekuchwa; akatwaa jiwe moja la mahali pale akaliweka chini ya kichwa chake, akalala usingizi pale pale).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.
More
Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/