Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022Mfano

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

SIKU 16 YA 31

Bwana, Mungu aliye hai, alijifunua kwa Yakobo akijitambulisha kama Mungu wa baba yake na babu yake. Ila Yakobo binafsi alikuwa bado hajamkiri Bwana kama Mungu wake. Alipomdanganya baba yake hakusema “Mungu wangu,” bali “Mungu wako” (27:20, Yakobo akasema, Kwa sababu Bwana, Mungu wako, amenifanikisha)! Baada ya ndoto akasema: Kweli Bwana yupo mahali hapa (m.16). Hata hivyo alikawia kumkiri kama Mungu wake. Ila akatoa ahadi: Mungu akiwa pamoja nami ... nami nikirudi kwa amani nyumbani kwa baba yangu, ndipo Bwana atakuwa Mungu wangu (m.20-21)!

siku 15siku 17

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022

Soma Biblia Kila Siku Januari/2022 ni mpango wa kusoma Biblia sehemu kwa sehemu kila siku kwa mwezi wa Januari pamoja na maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa kwa urahisi na kuendelea kutafakari neno la Mungu ulilosoma kwa situ husika. Katika mpango huu utasoma zaidi katika kitabu cha Mwanzo. Karibu kujiunga na mpango huu na usome bure.

More

Tungependa kuwashukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/