Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 9 YA 30

Ni muhimu kudumu katika kuomba: Dumuni sana katika kuomba, mkikesha katika kuomba huku na shukrani (m.2). Adumuye hivyo hubarikiwa na Mungu (mifano ni mingi, soma k.m. Lk 11:5-13 na 18:1-8). Tena, Mungu anataka tujifunze kuwa na uvumilivu katika kuomba. Anaweza kungoja kidogo kutoa tuombayo ili tujifunze kuendelea, yaani, kudumu katika maombi. Hilo tunajifunza pia katika mifano hiyo ya Injili ya Luka. Tuwakumbuke walio nje, yaani, wasio Wakristo: Enendeni kwa hekima mbele yao walio nje, mkiukomboa wakati (m.5). Ili Mungu apate kuwaingiza katika ufalme wake, tuukomboe wakati. Tunafanya hivyo kwa njia gani? Zingatia ilivyoandikwa katika m.6: Maneno yenu yawe na neema siku zote, yakikolea munyu, mpate kujua jinsi iwapasavyo kumjibu kila mtu.

Andiko

siku 8siku 10

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/