Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Kitabu cha Ufunuo wa Yohana kinahusu habari za wakati uliopo na ule ujao. Ni kitabu kinachotoa ujumbe wa tumaini lililopo na lijalo – kwa wanaomwamini Yesu Kristo. Hao ni wale wanaopata mateso kwa sababu ya imani yao, na kutokana na kutangaza ushindi wa Kristo dhidi ya uovu. Ushindi huu unaleta uzima wa milele. Mafundisho matatu ni ya muhimu kuzingatiwa: 1) Kristo anakuja tena. 2) Uovu utahukumiwa. 3) Wafu watafufuliwa kwa ajili ya hukumu, ndipo furaha ya uzima wa milele itafuata.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/