Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Yohana anaandika akiwa kifungoni Patmo. Pia kanisa lilipata mateso makali kutoka kwa waliompinga Kristo. Wakristo waliteswa kijamii, kisiasa na kiuchumi. Miongoni mwao alichinjwa. Yohana alifungwa kwa sababu alikataa kunyamazishwa ili asihubiri kuwa Kristo ni Mwokozi. Wakristo walisimama kidete. Wakashuhudia juu ya Yesu Kristo. Yohana akiwa matesoni alimwona Kristo (m.12-16). Nawe katika dhiki zako unahitaji kumtazama Yesu. Ushindi wa Kristo unatupa nguvu ya kuendelea kushuhudia popote tulipo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/