Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Kristo ana nguvu. Neno lake lina uweza mkuu. Ni maana ya mfano uliotumika katika m.16 kuhusu kinywa cha Yesu: Upanga mkali, wenye makali kuwili, ukitoka katika kinywa chake (Ebr 4:12 husema vivyo hivyo: Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo). Magonjwa, vifo, uchumi mbaya, ubadhirifu, na dhuluma vinaleta adha kwa watu wa leo. Mateso haya yanaweza kushawishi Wakristo wamwache Kristo. Lakini Kristo yupo, anasimama katikati ya hali uliyo nayo sasa. Vile vinara vya m.12-13 ni makanisa, kama ilivyoelezwa katika m.20: Vile vinara saba ni makanisa saba. Kristo anatembea katikati ya hivyo vinara, kama Yohana anavyoeleza katika m.13, Katikati ya vile vinara nikaona mtu mfano wa Mwanadamu. Kristo anatembea katikati ya makanisa. Ushindi wake upo hata sasa. Dhambi na matokeo yake havina nguvu mbele ya Kristo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/