Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Utajiri wa kiroho ni kulijua Neno la Kristo na si mashindano. Mateso ya imani hayaepukiki. Ni sehemu ya maisha ya kumfuata Kristo. Daima kuna kusongwa na wanafiki na wajumbe wa Ibilisi. Anayemwamini Kristo haogopi kufungwa kwa kuwa anamtetea Kristo. Kama unamfuata Kristo usihofu, usifadhaike. Jifunze kwa Kristo. Alikubali kufa kwa sababu ya kuutetea ukweli wa Mungu. Mateso yake yametuokoa. Umkazie macho Kristo hata uwapo katikati ya majaribu na mahangaiko. Heri wafu wafao katika BWANA.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/