Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Yohana anaagizwa kuandika barua kwa makanisa saba: Haya uyaonayo uyaandike katika chuo, ukayapeleke kwa hayo makanisa saba: Efeso, na Smirna, na Pergamo, na Thiatira, na Sardi, na Filadelfia, na Laodikia (1:11). Sasa ni nchi ya Uturuki. Namba 7 inahusu ukamilifu na utimilifu. Ni tabia na sifa ya Kristo tu. Roho saba ni Roho Mtakatifu. Roho Mtakatifu na Mwana ni chemchemi ya ukweli wote, kama Yesu anavyotukumbusha katika Yn 14, kwanza kuhusu yeye mwenyewe: Mimi ndimi … kweli (m.6), na kisha kuhusu Roho Mtakatifu: Ndiye Roho wa kweli (m.17). Waliompokea Kristo wanashuhudia Injili kwa wengine kama makuhani, kwa sababu Yesu Kristo alitufanya kuwa ufalme, na makuhani kwa Mungu (m.6). Kristo ni mtawala mwenye mamlaka yote, na ametushirikisha sisi mamlaka yake. Kifo chake msalabani na ufufuo wake vimempa mamlaka hayo. Tukio hili lazima litangazwe.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/