Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Paulo na Epafra wana juhudi nyingi katika maombi. Ndiyo kazi muhimu sana tukipenda kuwaimarisha waumini kwenye njia ya mbinguni. Juhudi ya hao pia huonyesha kuwa kulikuwa na shida fulani. Hasa usharika wa Laodikia una shida (unaweza kusoma zaidi katika Ufu 3:14-22). Kwa muda mrefu Wakristo wa Laodikia walianza kumweka Yesu Kristo pempeni. Ipi ni hazina kuu ya maisha yako? Usisahau ni wapi ulipopata wokovu wako, maana ni hatari sana kupoteza hazina ya mbinguni! Afadhali tuwe maskini hapo duniani kuliko kuipoteza hiyo.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/