Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Tikiko alitoka Asia, na aliongozana na Paulo katika safari yake ya tatu ya misheni. Walikutana Efeso, na kuanzia hapo walikuwa pamoja katika safari (Mdo 20:4, Watu hawa wakafuatana naye [Paulo], … na Tikiko na Trofimo watu wa Asia). Pia Onesimo anatumwa kwao. Onesimo alikuwa kwanza mtumwa wa Filemoni, Mkristo wa Kolosai; lakini alitoroka, akafika Rumi ambapo alimkuta Paulo akawa Mkristo. Kwa Onesimo, kwenda Kolosai ni sawa na kurudi tena kwa Filemoni, bwana wake. Lengo la Paulo kumtuma ni kuwafariji wote wawili (m.7-9, Tikiko, … atawaarifu mambo yangu yote; ambaye nimemtuma kwenu kwa sababu iyo hiyo, ili mjue mambo yetu, naye akawafariji mioyo yenu; pamoja na Onesimo, … Hao watawaarifu mambo yote ya hapa petu.) - Kwa Wakristo ni muhimu kutiana moyo. Tafakari Paulo anavyoshuhudia hiyo, akiandika kuhusu watu hao aliowataja: Walikuwa faraja kwangu (m.11b).
Andiko
Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/