Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 7 YA 30

Paulo anatufundisha jinsi tunavyopaswa kuishi ili tupate maisha ya kifamilia yenye amani na furaha. Haya yote yapo chini ya upendo. Ikiwa wanaume wanachukua shughuli za wanawake kama sheria ya nyumbani, upendo utakosa nafasi. Shughuli za wanawake zizingatiwe hasa na wanawake wenyewe, na shughuli za wanaume zizingatiwe hasa na wanaume wenyewe! Kwa hiyo neno lifuatalo ni kwa wanawake peke yao: Ninyi wake, watiini waume zenu, kama ipendezavyo katika Bwana (m.18). Wakati neno lifuatalo ni kwa wanaume peke yao: Ninyi waume, wapendeni wake zenu msiwe na uchungu nao (m.19). Maagizo haya yapo pamoja na maagizo kwa watoto na wazazi kwa ajili ya kutunza upendo kati ya wote nyumbani. Tuwavumilie watoto. Kipekee akina baba wanakumbushwa: Ninyi akina baba, msiwachokoze watoto wenu, wasije wakakata tamaa (m.21)!

siku 6siku 8

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/