Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Wakristo wa Kolosai wameteuliwa (m.12, Mmekuwa wateule wa Mungu, watakatifu wapendwao). Kwa njia gani na kwa kusudi gani? Jibu analitoa Yesu katika Yn 15:16 akisema, Si ninyi mlionichagua mimi, bali ni mimi niliyewachagua ninyi; nami nikawaweka mwende mkazae matunda; na matunda yenu yapate kukaa; ili kwamba lo lote mmwombalo Baba kwa jina langu awapeni. Wakristo wako tayari kuanza kutenda matendo mema, maana yapo tayari mioyoni mwao. Paulo anapenda kutukumbushia jambo hilo, maana ni muhimu kwamba matunda ya Roho Mtakatifu yapate nafasi nzuri katika maisha yetu. Hayo ni mapenzi ya Mungu, na ni baraka kwetu na kwa wengine wanaotendewa mamba mema kwa njia ya maisha yetu. Labda wengine wanapata kuokolewa kwa sababu ya kuona upendo wa Mungu ndani yetu!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/