Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Dhambi haiwezi kufanyika bila kupitia viungo vyetu, k.m. mkono au ulimi. Vinapotumika kutenda dhambi, Paulo anaviita “viungo vilivyo katika nchi”. Neno "vifisheni" si tafsiri nzuri. Ni afadhali kutafsiri "viache vife". Maana vile viungo havina ruhusa wala haki ya kumtawala aliyebatizwa, kwa sababu vimeshasulibishwa pamoja na Kristo, kama ilivyoandikwa katika Rom 6:6, Utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye [Yesu], ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena. Wakati vile viungo vinapotaka kutenda mabaya, tukumbuke kuwa nguvu ya dhambi imeshagongomewa msalabani, basi ibaki pale pale. Tumwache Yesu aifishe!
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/