Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 4 YA 30

Paulo anakaza umoja wetu na Yesu Kristo: Uhai wetu umefichwa na Kristo (m.3). Yaani, ukimtegemea Yesu kama Mwokozi wako, umefichwa katika yeye. Mungu hatakuona kama alivyokuona kwanza. Anamwona Yesu tu katika maisha yako. Ndivyo ulivyo wokovu wetu. Ndani ya Yesu shetani hana mamlaka tena. Ni mahali pa salama kabisa. Huwa tunavutwa na mambo ya dunia hii, lakini tukimtazama Yesu hatufuati mambo hayo, bali twamfuata Yesu. Ndiyo sababu ya Paulo kusema kama ilivyoandika katika m.1-2: Basi mkiwa mmefufuliwa pamoja na Kristo, yatafuteni yaliyo juu Kristo aliko, ameketi mkono wa kuume wa Mungu. Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi!

Andiko

siku 3siku 5

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/