Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

SIKU 3 YA 30

Waalimu wa uongo hawamtaki Yesu Kristo kuwa kichwa chao. Kwa hiyo Paulo anatuonya, Mtu asiwanyang'anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili; wala hakishiki Kichwa (m.18-19). Wanayotangaza ni uongo na hayana maana kabisa. Paulo anataka Wakristo watambue jambo hilo. Anawahubiria wokovu utokanao na Yesu ambaye ndiye Kristo, Mwokozi pekee. Waalimu wa uongo ni wengi, na hata moyo wetu unaweza kutudanganya. Kwa hiyo tunapaswa kupokea ukweli huo kutoka kwa Mungu ili tuweze kukutana na uongo bila kuanguka, bali kusimama katika imani ya kweli. Tusiongeze sheria za kibinadamu. Ukiwa na nafasi, utafute Mk 7:8-13 ukasome anayosema Yesu juu ya jambo hili.

siku 2siku 4

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021

Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/