Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021Mfano
Kufuatana na utu wetu tuliozaliwa nao hatumtaki Mungu. Ni kama kifo cha uhusiano wetu naye. Kifo kimeingia kwa njia gani? Jibu linapatikana katika m.13! Ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote. Uhai twapata kwa njia gani? Kwa njia ya Mungu kutusamehe makosa yetu! Dhambi zetu zote zimefutwa kabisa na Yesu Kristo, alipozichukua msalabani na kutulipia deni letu kwa kifo chake. Msamaha ulipatikana, Mungu akiisha kuifuta ile hati iliyoandikwa ya kutushitaki kwa hukumu zake, iliyokuwa na uadui kwetu; akaiondoa isiwepo tena, akaigongomea msalabani (m.14). Utu wa kale (mwili wa dhambi) hautoki ndani yetu tukiwa hapa duniani, lakini sasa upo chini ya mamlaka ya Yesu Kristo, maana aliugongomea msalabani na akashinda kifo! Tafakari habari njema iliyoandikwa katika Rum 6:6, Utu wetu wa kale ulisulibishwa pamoja naye, ili mwili wa dhambi ubatilike, tusitumikie dhambi tena.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Septemba 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Wakolosai, 2 Samweli na Ufunuo. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kuishukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz/