Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Kuna malipo kwa ubaya autendao mtu. Ila neno hili mtu asiporejea (m.12) laonyesha pia kwamba huwa Bwana anamwachia nafasi ya kuongoka. Kwa hiyo kupona malipo mabaya kunategemea uamuzi wa mtu mwenyewe. Akitambua ubaya, akatubu na kuuacha, atapona. Bali akijivunia uovu na kudumu ndani yake, atafananishwa na mtu anayejichimbia shimo la kujiangamiza nafsi yake. Madhara yake yatamrejea kichwani pake, Na dhuluma yake itamshukia utosini (m.16). Changamoto ya leo ni hii: Je, kuna lolote katika maisha yako ambalo lakuweka katika njia ya watenda mabaya? Tubu na kuacha.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz