Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 29 YA 30

Wakati fulani nilidhani sheria za nchi na mahakama hutoa haki. Siku moja nilishtakiwa kwa madai ya kusingiziwa. Nilionekana mwenye hatia. Kumbe wanadamu hawawezi kujua ukweli wa mioyo ya watu!! Mungu ajuaye mioyo kwa ukamilifu, ndiye pekee awezaye kutoka hukumu ya haki. Wanyenyekevu wake wapaswa kufarijika kwa ukweli huu. Bwana ni ngao yao. Atawaokoa – kama ilivyoandikwa katika m.10: Ngao yangu ina Mungu, awaokoaye wanyofu wa moyo. Kwa upande mwingine, wanaowatendea mabaya wenzao watetemeke mbele zake kwa hofu na kicho, kwani Bwana ni mwenye ghadhabu juu ya ubaya.

siku 28siku 30

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz