Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Yaaminika zaburi hii iliandikwa na Daudi. Adui alimsingizia uovu na kumtesa bila sababu. Nguvu ya adui ni kubwa (angalia jinsi Daudi anavyomlinganisha na simba katika m.2: asije akaipapura nafsi yangu kama simba). Lakini Daudi ana nguvu tofauti inayomshinda: Daudi ni mnyofu wa moyo na kuishi maisha safi, halafu anamwachia Mungu ahukumu kati yake na adui. Bwana ndiye pekee mlinzi kwa watendewao mabaya na mwamuzi wa haki tunaposingiziwa bila sababu. Mlipa kisasi anapaswa kuwa Mungu na si kazi yetu, kama ilivyoandikwa katika Kum 32:35-36, Kisasi ni changu mimi, na kulipa, wakati itakapoteleza miguu yao; maana siku ya msiba wao imekaribia, na mambo yatakayowapata yatafanya haraka. Kwa kuwa Bwana atawaamua watu wake, atawahurumia watumwa wake, aonapo ya kuwa nguvu zao zimeondoka, na ya kuwa habaki mtu, aliyefungwa wala asiyefungwa,. Kwa hiyo peleka maonevu dhidi yako kwa Mungu na mwache ahukumu.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz