Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Misri bado anaombolezewa. Nchi hii imejawa na kiburi hadi kutakiwa kueleza nani analingana naye; lakini umaarufu, uzuri na ukuu wake hautamsaidia lolote. Farao na watu wake wataangushwa na kulazwa pamoja na mataifa hayo mengine ambayo Mungu ameshayahukumu. Hali ya kutotahiriwa ni mfano wa kutomwamini Mungu. Hata mwenye tohara mwilini mwake akumbuke hiyo. Neno la Mungu linadhihirisha kwamba tohara yenyewe haitoshi kuleta ukombozi. Zingatia somo la leo kwa kulinganisha na Kol 2:11-13, Katika yeye [= Kristo] mmetahiriwa kwa tohara isiyofanyika kwa mikono, kwa kuuvua mwili wa nyama, kwa tohara ya Kristo. Mkazikwa pamoja naye katika ubatizo; na katika huo mkafufuliwa pamoja naye, kwa kuziamini nguvu za Mungu aliyemfufua katika wafu. Na ninyi mlipokuwa mmekufa kwa sababu ya makosa yenu na kutokutahiriwa kwa mwili wenu, aliwafanya hai pamoja naye, akiisha kutusamehe makosa yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz