Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 27 YA 30

Zaburi hii huonyesha kuwa wanadamu ni wapotofu. Katika hali hiyo wanapanga maovu, na ndimi zao hunena uongo. Tena hujihesabu kuwa washindi na kuona waamini hawana Mungu. Lakini hivyo hukaribisha hukumu ya Mungu, maana litakalosimama imara milele ni neno lake. Maneno ya Bwana ni maneno safi, Ni fedha iliyojaribiwa kalibuni juu ya nchi; Iliyosafishwa mara saba (m.6)! Mungu husimama upande wa wanenewao na kutendewa ubaya. Ni kusudi lake siku zote kuwaokoa. Linganisha na Mungu anavyosema katika Kut 3:7-9, Hakika nimeyaona mateso ya watu wangu walioko Misri, nami nimekisikia kilio chao kwa sababu ya wasimamizi wao; maana nayajua maumivu yao; nami nimeshuka ili niwaokoe na mikono ya Wamisri, niwapandishe kutoka nchi ile, hata nchi njema, kisha pana; nchi ijaayo maziwa na asali; hata mahali pa Mkanaani, na Mhiti, na Mwamori, na Mperizi, na Mhivi, na Myebusi. Basi, tazama, kilio cha wana wa Israeli kimenifikilia; tena nimeyaona hayo mateso ambayo Wamisri wanawatesa. Huku tukitambua kuwa udhalimu ni sehemu ya dunia, tufarijike kwa neno hili kuwa Bwana atawalinda watu wake dhidi ya waovu. Tumtegemee tukimsifu pamoja na mtunzi wa zaburi: Wewe, Bwana, ndiwe utakayetuhifadhi, utatulinda na kizazi hiki milele (m.7).

siku 26siku 28

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz