Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu (m.8). Walimu wa dini ya Kiyahudi (wanatheolojia) walikuwa wametunga sheria nyingi za ziada kwa kufafanua sheria za Musa, kama m.3-5 inavyoonyesha: Mafarisayo na Wayahudi wote wasiponawa mikono mpaka kiwiko, hawali, wakishika mapokeo ya wazee wao; tena wakitoka sokoni, wasipotawadha, hawali; na yako mambo mengine waliyopokea kuyashika, kama kuosha vikombe, na midumu, na vyombo vya shaba. Basi wale Mafarisayo na waandishi wakamwuliza, Mbona wanafunzi wako hawaendi kwa kuyafuata mapokeo ya wazee, bali hula chakula kwa mikono najisi? Mafafanuzi haya kwa Wayahudi yalihesabika kuwa Neno la Mungu sawasawa na sheria ya Musa. Lakini jambo hili Yesu alilikanusha. Maana utakatifu wao ukiwa tofauti na mkazo wa amri ya Mungu, iliwafanya kuwa wanafiki, wakapotoka. Kwa hiyo Yesu akawaambia, Isaya alitabiri vema juu yenu ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa, Watu hawa huniheshimu kwa midomo Ila mioyo yao iko mbali nami; Nao waniabudu bure, Wakifundisha mafundisho Yaliyo maagizo ya wanadamu, Ninyi mwaiacha amri ya Mungu, na kuyashika mapokeo ya wanadamu (m.6-8). Je, wanatheolojia wa leo wakifundisha kinyume cha Neno la Mungu tutawafuata?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz