Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Ametenda mambo yote vema (m.37). Ili kuelewa vizuri zaidi habari hizi za uponyaji tujue kwamba ”watoto” anaowazungumzia Yesu katika m.27 ni mfano wa Wayahudi (Akamwambia, Waache watoto washibe kwanza; maana si vizuri kukitwaa chakula cha watoto, na kuwatupia mbwa). Yesu anasema wana haki ya kwanza kusikia Injili (ling. Mt 15:24 anaposema, Sikutumwa ila kwa kondoo waliopotea wa nyumba ya Israeli). Neno ”mbwa” lingetakiwa kutafsiriwa "mbwa wadogo". Si mbwa wanaozungukazunguka, bali wako nyumbani kwa mtu. Hao ni mfano wa watu wasio Wayahudi. Yesu ”akaugua”, yaani anaona uchungu kwa ajili yule bubu. Kwanza anamfanyia vitendo ili aelewe Yesu anataka kumfanyia nini. Ndipo Yesu anamponya kwa neno.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz