Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Huyawazi yaliyo ya Mungu, bali ya wanadamu (m.33). Petro alikuwa ametambua kwamba Yesu ni Kristo, yaani yule Mwokozi wa taifa la Israeli ambaye ametabiriwa katika Agano la Kale. Lakini mawazo ya Petro juu ya Kristo ni kinyume cha mawazo ya Mungu. Petro na Wayahudi walio wengi waliona kwamba Kristo atawashinda maadui wao wote na kuleta amani kwa ulimwengu mzima. Ndiyo, Yesu ni amani yetu, lakini kuna unabii mwingine juu ya Kristo ambao ilibidi utimizwe kabla ya hayo. Umefafanuliwa namna hii katika Isa 53:3-6, Alidharauliwa na kukataliwa na watu; Mtu wa huzuni nyingi, ajuaye sikitiko; Na kama mtu ambaye watu humficha nyuso zao, Alidharauliwa wala hatukumhesabu kuwa kitu. Hakika ameyachukua masikitiko yetu, Amejitwika huzuni zetu; Lakini tulimdhania ya kuwa amepigwa, Amepigwa na Mungu, na kuteswa. Bali alijeruhiwa kwa makosa yetu, Alichubuliwa kwa maovu yetu; Adhabu ya amani yetu ilikuwa juu yake, Na kwa kupigwa kwake sisi tumepona. Sisi sote kama kondoo tumepotea; Kila mmoja wetu amegeukia njia yake mwenyewe; Na Bwana ameweka juu yake Maovu yetu sisi sote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz