Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Kwa kufuata sheria zote za wazee (kama m.3 unavyosema walifanya), Wayahudi walidhani wataweza kufikia hali ya kuwa safi mbele ya Mungu. Lakini Yesu anafundisha leo kwamba haiwezekani, maana maovu yanatoka ndani ya mioyo ya watu (m.20-23: Kimtokacho mtu ndicho kimtiacho unajisi. Kwa maana ndani ya mioyo ya watu hutoka mawazo mabaya, uasherati, wivi, uuaji, uzinzi, tamaa mbaya, ukorofi, hila, ufisadi, kijicho, matukano, kiburi, upumbavu. Haya yote yaliyo maovu yatoka ndani, nayo yamtia mtu unajisi). Na mioyo haiwezi kusafishwa kwa sheria hizo. Utabaki kuwa usafi wa nje tu. Kwa sababu hiyo Yesu alimfundisha Nikodemo kuwa lazima tuzaliwe upya, tuzaliwe kwa Roho. Bila hivyo hatuwezi kuuingia Ufalme wa Mungu! Inawezekanaje kuzaliwa upya? Tafakari Mungu anayosema katika Eze 36:25-28, Nami nitawanyunyizia maji safi, nanyi mtakuwa safi; nitawatakaseni na uchafu wenu wote, na vinyago vyenu vyote. Nami nitawapa ninyi moyo mpya, nami nitatia roho mpya ndani yenu, nami nitatoa moyo wa jiwe uliomo ndani ya mwili wenu, nami nitawapa moyo wa nyama. Nami nitatia roho yangu ndani yenu, na kuwaendesha katika sheria zangu, nanyi mtazishika hukumu zangu, na kuzitenda. Nanyi mtakaa katika nchi ile niliyowapa baba zenu, nanyi mtakuwa watu wangu, nami nitakuwa Mungu wenu. Kumbuka pia ilivyoandikwa katika 1 Yoh 1:7, Tukienenda nuruni, kama yeye alivyo katika nuru, twashirikiana sisi kwa sisi, na damu yake Yesu, Mwana wake, yatusafisha dhambi yote.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz