Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Somo hili linatuonyesha kuwa Yesu anajali matatizo yetu ya kimwili. Baba yetu wa Mbinguni anaguswa rohoni akiona tuna njaa, tumekosa nguo au tukiwa wagonjwa (ukiwa na nafasi unaweza kulinganisha na Mt 6:25-34). Kwa hiyo tunaweza kumwomba kwa ujasiri tukiwa taabuni. Na tukiwa na raha, tusisahau kumshukuru na kuwahurumia wenye mahitaji! Siku hizi Yesu hayupo katikati yetu kama wakati ule. Hata hivyo bado anaendelea kutenda kazi yake ya huruma miongoni mwetu kwa kupitia sisi wafuasi wake. Sisi ni mikono yake, kama tunavyojifunza kutokana na habari ya m.6: Yesu akawaagiza mkutano waketi chini; akaitwaa ile mikate saba, akashukuru, akaimega, akawapa wanafunzi wake wawaandikie; wakawaandikia mkutano.
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz