Chapa ya Youversion
Ikoni ya Utafutaji

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

SIKU 22 YA 30

Ezekieli anaagizwa kutabiri hukumu juu ya mfalme wa Misri, nchi yake, na wote walioambatana naye. Farao anafananishwa na joka kubwa mwenye kuonyesha kiburi cha utawala na umiliki wa mto Nile. Mungu anachukizwa na yeyote anayejifanya kuwa Muumba, kama ilivyoelezwa katika m.3 na 9: Bwana MUNGU asema hivi; Tazama, mimi ni juu yako, Ewe Farao, mfalme wa Misri, joka kubwa aoteaye kati ya mito yake, aliyesema, Mto wangu ni wangu mwenyewe, nami nimeufanya kwa ajili ya nafsi yangu. Hukumu yake juu ya Wamisri itadumu miaka 40, kisha atawarejeza, ila watabaki kuwa duni. Hiyo itakuwa fundisho muhimu kwa watu wa Mungu siku zote: Wasiwategemee watu na mamlaka yao jinsi walivyowahi kufanya: Watu wote wakaao Misri … wamekuwa mwanzi wa kutegemewa kwa nyumba ya Israeli. … nao walipokutegemea, ulivunjika … [ufalme wa Wamisri] hautakuwa tena tumaini la nyumba ya Israeli (m.6b-7 na 16). Tuzingatie kwamba ni heri kumkimbilia Bwana kuliko kuwatumainia wanadamu (Zab 118:8).

siku 21siku 23

Kuhusu Mpango huu

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021

Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu

More

Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz