Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Watoto wadogo ni watoto wenye umri hadi miaka 12. Pia walikuwepo watoto wachanga: Wakamletea na watoto wachanga ili awaguse (Lk 18:15). Hapa twajifunza mambo muhimu juu ya watoto kama hao: 1. Wanahitaji wokovu, wanahitaji kupokea ufalme wa Mungu. Wanahitaji kubarikiwa. Kwa sababu hiyo Yesu alichukizwa alipoona wanafunzi wakiwazuia! 2. Wanaweza kabisa kupokea wokovu, kupokea ufalme wa Mungu. Kama wasingaliweza Yesu asingaliwabariki. Tena namna yao ya kupokea ni mfano kwa watu wazima. Hivyo ye yote asiyeukubali ufalme wa Mungu kama mtoto mdogo hatauingia kabisa (m.15). Je, umejinyenyekeza kwa Yesu? Mungu huwapinga wajikuzao, bali huwapa neema wanyenyekevu (Yak 4:6).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz