Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Wakati mwingine mzazi hawezi kujua mtoto wake ana haja zipi bila mtoto mwenyewe kutamka. Yesu alijua tayari haja ya yule kipofu kwamba anataka apate kuona. Hata hivyo alimtaka mwenyewe atamke. Vilevile kwetu Wakristo. Baba yetu wa Mbinguni anajua tayari haja zetu zote. Hata hivyo anataka tumwambie ili tupatapo lile tunalohitaji tutambue wazi kuwa yeye ndiye aliyetupa! Ombeni, nanyi mtapewa (Mt 7:7)! Yaani, tusipoomba tutakosa kitu ambacho tungeweza kupata kwa kuomba. Basi, msijisumbue kwa neno lo lote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu. Na amani ya Mungu, ipitayo akili zote, itawahifadhi mioyo yenu na nia zenu katika Kristo Yesu (Flp 4:6-7).
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz