Soma Biblia Kila Siku Juni 2021Mfano
Somo linaonyesha jinsi mji wa Tiro ulivyojisifia juu ya ukamilifu wa uzuri wake, ukisema: Mimi ni ukamilifu wa uzuri (m.3). Umevutia wafanya biashara wengi wanaotumikia utajiri wa mji kwa kuuletea vitu vingi vizuri vya thamani kutoka mataifa mengi. Lakini angalia kwamba somo ni wimbo wa maombolezo juu ya Tiro. Mungu anamwambia Ezekieli, Wewe, mwanadamu, mfanyie Tiro maombolezo (m.2). Ina maana kwamba uzuri wake mji wa Tiro, mafanikio yake yote, na hadhi kubwa uliyo nayo mji huo havitazuia anguko utakalopata. Hili ni onyo kubwa kwetu sote hata leo. Zingatia Yesu anavyoliambia kanisa la Laodikia, Kwa kuwa wasema, Mimi ni tajiri, nimejitajirisha, wala sina haja ya kitu; nawe hujui ya kuwa wewe u mnyonge, na mwenye mashaka, na maskini, na kipofu, na uchi. Nakupa shauri, ununue kwangu dhahabu iliyosafishwa kwa moto, upate kuwa tajiri, na mavazi meupe upate kuvaa, aibu ya uchi wako isionekane, na dawa ya macho ya kujipaka macho yako, upate kuona (Ufu 3:17-18). Je, wewe ni tajiri kwa Mungu?
Andiko
Kuhusu Mpango huu
Soma Biblia Kila Siku Juni 2021 ni mpango mzuri wa kusoma Biblia kila siku sehemu kwa sehemu hasa katika kitabu cha Marko na Ezekieli. Mpango huu una maelezo mafupi yatakayokusaidia kuelewa zaidi Neno la Mungu. Karibu kujiunga na mpango huu
More
Tungependa kumshukuru Soma Biblia kwa kutoa mpango huu. Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: http://www.somabiblia.or.tz